Mount akili yake aiwaza Man United

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Taarifa za ndani zinaeleza kiungo wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza Mason Mount anataka kujiunga na klabu ya Manchester United katika dirisha kubwa majira haya ya joto.


Mason Mount amekua hapendezwi na yeye kukosa nafasi ndani ya kikosi cha Chelsea mara kwa mara msimu huu, Hivo ameonekana kuhitaji changamoto nyingine nje ya klabu ya Chelsea na sehemu pekee ambayo mchezaji huyo anataka kwenda ni klabu ya Manchester United.


Klabu ya Manchester United nayo inamfukuzia mchezaji huyo na kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag ndio anavutiwa na kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza, Lakini changamoto inakuja kwa Chelsea ambao inaelezwa wameweka dau kubwa sana kwa timu ambayo itahitaji huduma ya kiungo huyo.


Mason Mount ni kijana alifuzu kutoka akademi ya Chelsea inayofahamika kama Cobham kabla ya kuanza kucheza timu ya wakubwa hivo Chelsea ni timu yake ya utotoni, Lakini kwasasa anataka changamoto nyingine na klabu hiyo ipo tayari kumuuza kama tu timu inayomtaka itafika dau wanalolitaka.


Kiungo Mount atakumbukwa ndani ya klabu ya Chelsea kwa msimu wake wa 2020/21 ambapo alikua kwenye msimu bora zaidi, Huku pia akifanikiwa kutwaa taji la ligi ya mabingwa ulaya msimu huo lakini misimu miwili mbele ameonekana kutokupata nafasi ndani ya timu hiyo mara kwa mara na ndio sababu ya kutaka kuondoka.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post