Morrizon atuma maombi wizara ya ndani kubadili uraia wake kuwa mtanzania

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Winga wa Yanga Bernard Morrison amedhamiria kuwa Mtanzania baada ya kuanza mchakato wa kubadili uraia wake


Morrison amethibitisha kuwa alituma maombi Wizara ya mambo ya ndani tangu mwaka 2021 akiomba uraia wa Tanzania ili aweze kuichezea timu ya Taifa


Morrison alitua nchini kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2019 akiwa miongoni mwa wachezaji wa mwanzo kusajiliwa na GSM, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said akifanikisha kumleta nchini


Morrison hajawahi kuficha mapenzi yake kwa nchi ya Tanzania na mara kadhaa amenukuliwa akisema anatamani kuishi Tanzania hata pale atakapostaafu kucheza soka


Nyota huyo mwenye vituko vingi hatakuwa mchezaji wa kwanza kuomba uraia wa Tanzania katika misimu ya karibuni


Mshambuliaji wa Simba Kibu Denis alibadili uraia wa DR Congo mwanzoni msimu wa 2021/22 na kuwa Mtanzania sasa akiichezea timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post