VIDEO: Morrison amvalisha msemaji Simba medali ya CAF

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Katika hali ya utani winga wa Klabu ya Yanga, Bernard Morrison 'BM3' amemtamanisha medali ya kombe la Shirikisho Afrika, Meneja Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally kwa kumvalisha na kumvua.


Morrison aliyekipiga Klabu ya Simba msimu uliopita, katika tukio hilo la aina yake lilomfanya Ahmed na wadau wengine akiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat’ walioketi karibu yao kuangua kicheko lilifanyika kwa muda mfupi kabla ya kumvua tena kisha kuivaa tena mwenyewe.


Tukio hilo limetokea leo Jumatatu Juni 5,2023 Ikulu Dar es Salaam, wakati wakishiriki chakula cha usiku na timu ya Yanga kikiandaliwa na Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni kuwapongeza kwa hatua waliyofikia ya kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).


Wachezaji wa Yanga walishiriki hafla hiyo iliyofanyika Ikulu ikiwakusanya viongozi mbalimbali wadau wa mchezo wa soka nchini ikiwemo Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia.


Yanga iliwasili jana usiku ikitokea nchini Algeria walikoenda kucheza fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao US Alger waliotawazwa kuwa mabingwa wakibebwa na sharia ya bao la ugenini.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post