Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuber Homera amesema kuwa kuelekea mchezo wa marudiano kati ya Mbeya City dhidi ya Mashujaa hatua ya mtoano(play off) hakutakuwa na kiingilio ili kutoa nafasi kwa mashabiki kuingia kwa wingi uwanjani na kuipa hamasa timu yao
Homera amesema baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 3-1 na Mashujaa Fc katika mchezo wa kwanza wa play-off uliopigwa mkoani Kigoma, wanapaswa kushikamana kipindi hiki ambacho Mbeya City inapatia mazingira magumu ya kupambana ili kusalia ligi kuu Tanzania bara
"Matokeo ya kule Kigoma sio mazuri,inapaswa tushirikiane kwa pamoja ili kuinusuru timu yetu, niwaombe sana mashabiki wa soka na wadau tufike kwa wingi uwanjani, hakutakuwa na kiingilio yaani bureee,tuujaze uwanja wa Sokoine ili tupindue matokeo," alisema Homera
Mchezo wa marudiano Kati ya Mbeya City dhidi ya Mashujaa hatua ya Play off umepangwa kuchezwa June 22, 2023 katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
Mbeya City wanahitaji kupata ushindi wa goli 2-0 baada ya mchezo wa kwanza kupoteza kwa mabao 3 - 1 Lake Tanganyika Kigoma.
Post a Comment