Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele jana aliisaidia DR Congo kupata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Gabon katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2023
Mayele aliyeingia kwenye dakika ya 74, alifunga bao la pili la DR Congo kwenye dakika ya 83 baada ya kuwachambua walinzi wa Gabon kabla ya kuujaza mpira kimiani
Baada ya kuuweka mpira kimiani Mayele alishangilia kwa staili yake ya kutetema huku wachezaji wote wa DR Congo wakiungana nae kutetema
Jana nyota nane wa Yanga walikuwa uwanjani kuzitumikia timu zao za Taifa
Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Bacca na Mudathir Yahya waliitumikia Taifa Stars katika mchezo dhidi ya Niger uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na Tanzania kushinda bao 1-0
Khalid Aucho akaitumikia Uganda katika mchezo dhidi ya Algeria wakati Djigui Diarra akiwa langoni katika mchezo dhidi ya Congo (Brazaville)
Stephane Aziz Ki akaanza katika mchezo dhidi ya Cape Verde
Post a Comment