Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Dakika 45 za kibabe kwenye kipindi cha pili zimeihakikishia Yanga kuondoka na alama moja katika uwanja wa Sokoine baada ya sare ya mabao 3-3 dhidi ya Mbeya City
Salum Abubakar 'Sure Boy' na Bernard Morrison ndio waliohakikishia Yanga alama moja ya kuongezea juu ya alama 74 za ubingwa Yanga ikishuhudiwa ikitoka nyuma kwa mabao 3-0
Sangija na Richardson Ngondya walifunga mabao ya Mbeya City ambayo mpaka dakika ya 64 ilikuwa mbele kwa mabao 3-0 kabla ya Morrison kufunga bao la kwanza la Yanga kwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 65
Sure Boy akaongeza la pili kwenye dakika ya 69 kabla ya Morrison kuisawazishia Yanga kwenye dakika za jiooooni kabisa
Katika mchezo huo winga Jesus Moloko alitolewa nje kwa kadi nyekundu sambamba na Nassor Maulid wa Mbeya City baada ya wachezaji hao kupigana
Post a Comment