Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) limerejea tena kwenye makabati ya Yanga pale Jangwani baada ya kuichapa Azam Fc bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Mkwakwani
Alikuwa ni Kennedy Musonda aliyeihakikishia Yanga medali ya dhahabu ya tatu msimu huu akifunga bao pekee kwa kichwa kwenye dakika ya 13
Haikuwa mechi rahisi kutokana na mazingira yaliyokuwa yakiwakabili Yanga, mechi mfululizo na mchezo kupigwa saa tisa mchana jua likiwa kali
Yanga ilikuwa bora zaidi kwenye kipindi cha kwanza huku ikiwa imara zaidi katika kujilinda na kutumia mashambulizi ya kushitukiza katika kipindi cha pili
Ndio! habari ndio hiyo, bingwa wa Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na kombe la FA ni Yanga kwa msimu wa pili mfululizo
Post a Comment