Matchday : Usm Alger vs Yanga Itazame hapa

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Yanga iko tayari kwa mchezo wa pili wa fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger ambao utapigwa leo saa nne usiku katika uwanja wa July 05


Kikosi cha Yanga kilikamilisha maandalizi ya mwisho katika uwanja huo jana, kazi ni moja leo kusaka ushindi wa angalau mabao mawili ambao utawahakikisha mabingwa hao wa Tanzania ubingwa wa Shirikisho Afrika


Ni mchezo ambao Yanga haina cha kupoteza. Tayari iko nyuma kwa mabao 2-1 hivyo ni wazi Kocha Nasreddine Nabi atatumia kikosi chake bora zaidi katika kushambulia


Matokeo yoyote katika mchezo huo hayawezi kufuta mafanikio ya Yanga waliyopata katika michuano hiyo


Wachezaji wa Yanga watavaa medali za CAF leo, kama watakuwa mabingwa watavaa medali za dhahabu lakini wakiukosa ubingwa watavaa medali za silver


Yanga ndio timu ya kwanza Afrika Mashariki kufika fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa Yanga wanastahili pongezi kwa mafanikio haya


Kwa hatua waliyofikia ni kama wameshakula ng'ombe mzima, mchezo wa leo ni kumalizia mkia tu!


Wachezaji wamepambana tangu mchezo wa kwanza hadi fainali, matumaini ya Wananchi ni kuwa leo hawatashindwa kukamilisha kazi ndogo iliyobaki ili watwae ubingwa na kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu


Ni mechi kubwa, mechi ya heshima, mechi ya fainali ambayo wachezaji wanafahamu thamani yake na WAKO TAYARIMechi itakuwa LIVE kwenye app yetu bofya hapa kuidownload bure sasa ili usipitwe na mechi hii

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post