Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo inatupa karata muhimu uwanja wa Benjamin Mkapa ukiwa ni mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon 2023 dhidi ya Niger
Tanzania inahitaji kushinda leo ili kuweka hai matumaini ya kufuzu huku ikiomba Uganda ipoteze mchezo dhidi ya Algeria ambao utapigwa huko Cameroon
Algeria tayari imefuzu wakati Tanzania, Uganda na Niger bado zinachuana kuwania nafasi ya pili
Tanzania inashika nafasi ya pili kundi F ikiwa na alama nne sawa na Uganda wakati Niger inashika nafasi ya nne ikiwa na alama mbili
Mechi ya mwisho kwa Tanzania ni ugenini dhidi ya Algeria hivyo kufanya mchezo wa leo dhidi ya Niger kuwa lazima kushinda na kwenda kusaka angalau alama moja huko Algeria
Mchezo utapigwa saa 10 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Post a Comment