Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Leo msimu wa mashindano 2022/23 unahitimishwa mkoani Tanga kwa mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Yanga dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa saa 9 Alasiri katika uwanja wa Mkwakwani
Baada ya mchezo huo usiku kutakuwa na tukio la utowaji tuzo kwa waliofanya vizuri Ligi Kuu, Ligi ya Wanawake na kombe la FA msimu wa 2022/23
Huu unaweza kuwa msimu bora zaidi kwa Yanga kama itaweza kutwaa kombe la FA na utakuwa msimu wa pili mfululizo kushinda taji hilo
Baada ya kutwaa Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na kucheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC), Wananchi wana matarajio leo wanaweza kuongeza taji la tatu kabatini kama walivyofanya msimu uliopita
Hata hivyo wanakutana na Azam Fc ambayo ubingwa wa FA yatakuwa mafanikio yao makubwa zaidi kuyapata katika misimu ya hivi karibuni
Yanga inashuka uwanjani leo bila ya mshambuliaji wake kinara wa mabao Fiston Mayele ambaye yuko kwenye majukumu ya timu ya Taifa
Mayele na Stephane Aziz Ki waliondoka nchini mapema jana kujiunga na timu za Taifa baada vyama vya soka DR Congo na Burkina Faso kugomea maombi ya Yanga kuwatumia wachezaji hao leo
Huenda Clement Mzize na Kennedy Musonda leo wakaongoza safu ya ushambuliaji huku kukiwa na uwezekano wa winga Benard Morrison kuanza wakati Jesus Moloko akikosekana akitumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo dhidi ya Mbeya City Mechi itakuwa live kwenye App yetu bofya hapa kuidownload sasa ili uweze kuitazama mechi hii kwenye simu yako
Post a Comment