Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Magoli mawili kutoka kwa Kiungo wa Man City, Ilkay Gundogan yametosha kuwapa Man City ushindi wa mabao 2-1 na kuwapa Ubingwa wa FA mbele ya watani wao wa jadi Manchester United mchezo wa Fainali uliopigwa Uwanja wa Wembley.
City walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya kwanza tu ya mchezo kabla ya Bruno Fernadez kuisawazisha Man United kwa mkwaju wa Penati dakika ya 33 ya mchezo.
Gundogan kwa mara nyingine aliwarudisha City katika uongozi kwa bao lake la dakika ya 51 na kuwapa uongozi Man City wa mabao 2-1.
Mpaka dakika 90 zinakamilika City wanafanikiwa kunyakua taji la pili msimu huu huku wakiwa karibu kabisa kuandika rekodi ya kunyakua mataji matatu iwapo wataibuka mabingwa dhidi ya Inter Milan katika mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Post a Comment