Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Nadhani unalikumbuka lile kundi linaloundwa na wadau fulani hivi wa mpira ambao ni mashabiki wa Simba ambalo lilitikisa sana miaka kadhaa hapo nyuma.
Jamaa walikuwa maarufu sana ndani ya Simba kutokana na mchango mkubwa waliokuwa wanautoa katika timu hiyo hasa wa kifedha pale mambo yalipokuwa hayaiendei vizuri hasa katika ushiriki wake wa mashindano tofauti au wakati wa usajili.
Enzi zile ilikuwa ukisikia hilo kundi linatajwa tu basi ujue kuna kilio wameshakiacha mahali iwe kwa kuchukua mchezaji kipenzi katika timu fulani au kupata ushindi katika mechi dhidi ya mtani wake.
Nyakati zikasogea yakaja masuala ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji, jamaa wakapambana na wakashiriki vya kutosha katika mchakato na wakafanikiwa kuwemo katika chombo cha juu cha uongozi wa klabu hiyo.
Hata hivyo, baadaye mambo yakaanza kugeuka taratibu na nguvu ya lile kundi ikaanza kupotea katika namna tofauti.
Mkosi mkubwa kwa lile kundi ulikuwa ni kifo cha yule mfanyabiashara tajiri ambaye anatajawa kwamba huwa alikuwa na misimamo mizito ndani ya vikao vya klabu na alikuwa hayumbishwi kwani mfukoni alikuwa vizuri sana.
Baada ya hapo tukaanza kusikia mmojammoja akiondoka katika mfumo kwa njia yake jambo ambalo wengi hawakulitegema.
Wengine walijiengua wenyewe wakisema wameitumikia klabu kiasi cha kutosha lakini kuna wale ambao waliwekwa kando kwa kutopata uteuzi katika kile chombo chenye mamlaka ya kuendesha timu.
Na inasemekana mchakato wa kuliweka kando moja kwa moja unaendelea na sasa umegeukia kwenye upande wa timu ambapo utagusa hata wale walioingia kwa kuletwa na wanachama wa lile kundi.
Unaweza usielewe kwa haraka lakini siku kadhaa zijazo, lile kundi litabakia historia ndani ya Simba, labda liingie msituni kujipanga upya kimyakimya.
Chanzo: Mwanaspoti
Post a Comment