Ligi ya Vijana U20 kuanza Juni 21

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar wamepangwa Kundi A katika Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 inayotarajiwa kuanza Juni 21 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.


Katika Kundi hilo, A Mtibwa Sugar ya Morogoro ipo pamoja na Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani, Mbeya City ya Mbeya na Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi.


Kundi B linaundwa na Yanga SC ya Dar es Salaam, Polisi Tanzania ya Kilimanjaro, Dodoma Jiji ya Dodoma na Tanzania Prisons ya Mbeya, wakati Kundi C kuna Coastal Union ya Tanga, Geita Gold ya Geita, Singida Big Stars ya Singida na KMC ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.


Kundi D linawakutanisha Simba SC na Azam FC zote za Dar es Salaam, Ihefu SC ya Mbarali mkoani Mbeya na Kagera Sugar ya Bukoba.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post