Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc wanatajwa kuwa mbioni kukamilisha usajili wa mshambuliaji Leandre Essomba Willy Onana kinara wa mabao ligi kuu ya Rwanda msimu huu
Onana yuko jijini Dar es salaam tangu juzi wakala wake akidokeza kuwepo kwa mazungumzo baina yake na mabosi wa Simba
Straika huyo wa Rayon Sports ndiye kinara mabao kwa msimu wa 2022-23, alitikisa nyavu mara 16 kwenye ligi ya Rwanda
Ikumbukwe Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira ametaka michakato yote ya usajili ikamilishwe mwezi huu ili awe na wachezaji wake wote pale timu itakapoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/24
Juzi katika mahojiano na chombo kimoja cha habari, Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu alisema watasajili wachezaji watano wa kigeni kwa ajili ya kuimarisha maeneo yote yenye mapungufu
Post a Comment