Jezi ya Mkude kuwekwa kabatini Simba

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Klabu ya Simba imestaafisha jezi namba 20 iliyokuwa ikivaliwa na aliyekuwa kiungo wake Jonas Gerald Mkude


Uamuzi huo ni sehemu ya heshima ambayo Simba imeamua kumpa nyota huyo baada ya kuitumikia klabu kwa miaka 13


Mkude ambaye alitokea kwenye shule ya vijana ya Simba SC na kudumu katika kikosi cha wakubwa kwa takribani miaka 13 ameondoka klabuni hapo baada ya mkataba wake kufikia ukomo


Jezi namba 20 haitakuwepo msimu ujao hadi pale atakapopatikana mhitimu mwingine mwenye kuakisi kile ambacho Mkude amefanya klabuni hapo


Aidha klabu hiyo imepanga kumfanyia makubwa Mkude ikiwa ni kumuaga kwa heshima siku ya Simba Day 2023 huku ikimpa nafasi ya kurejea klabuni hapo baada ya maisha ya kucheza mpira kama ilivyo kwa Mussa Hassan Mgosi

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post