Huyu hapa mrithi wa manula Simba waanza mchakato wa kumpata - EDUSPORTSTZ

Latest

Huyu hapa mrithi wa manula Simba waanza mchakato wa kumpata

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Klabu ya Simba inatarajiwa kumsajili mlinda lango raia wa Brazil Caique Luiz Santos da Purificacao anayecheza klabu ya Ypiranga FC


Baada ya kuachana na Beno Kakolanya huku mlinda lango namba moja Aishi Manula akitarajiwa kuwa nje kwa miezi minne baada ya kufanyiwa upasuaji Afrika Kusini, Simba imelazimika kusajili mlinda lango mwingine


Caique mwenye umri wa miaka 25, akiwa amezaliwa Julai 31, 1997 katika mji wa Salvador huko Brazili kwa sasa anaichezea Ypiranga RS inayoshiriki Ligi ya Campeonato Brasileiro Serie C, sawa na First League hapa Tanzania akiwa kipa namba moja


Kipa huyo mwenye urefu wa futi 6 na inchi 5 alikulia kwenye akademi ya ES Victoria mwaka 2016, kabla ya kuitema na kwenda CSA ya Brazil sambamba na Ermis Aradippou ya Cyprus na Rochester NY ya Marekani kwa nyakati na misimu tofauti


Caique alikuwa kipa namba moja wa kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 (Brazil U-20), mwaka 2016 na 2017 kikishiriki michuano mbali mbali ya kimataifa kuonyesha kwamba ni mzoefu wa kutosha


Wakati akiwa kwenye kikosi hicho cha timu ya taifa alikuwa na nyota wengine wanaowika kwa sasa kwenye soka duniani wakiwemo Richarlison de Andrade wa Tottenham, Douglas Luiz wa Aston Villa, Lucas Paqueta wa West Ham na Gabriel Magalhes wa Arsenal


Awali Simba ilihusishwa kumuwania mlinda lango wa Al Hilal Issa Fofana lakini imekuwa ngumu kupata huduma yake baaada ya Al Hilal kugoma kumuuza



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz