Hii ndio hatma ya Mane Bayern Munich - EDUSPORTSTZ

Latest

Hii ndio hatma ya Mane Bayern Munich

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Sadio Mane amethibitisha kuwa atabaki Bayern Munich licha ya klabu hiyo kuonyesha nia ya kumsajili Harry Kane.


Tottenham wamekataa dau la kwanza la Bayern la pauni milioni 70 kwaajili ya kumnunua Kane, ambaye atafikisha miaka 30 mwezi ujao, lakini mabingwa hao wa Bundesliga wanatarajiwa kuwasilisha ofa ya pili hivi karibuni.


Mane, 31, amekuwa na wakati mgumu tangu ajiunge na Bayern kutoka Liverpool mwaka mmoja uliopita, kutokana na jeraha la mguu ambalo lilimweka nje kwa muda mrefu na akakosa fainali za Kombe la Dunia Qatar, mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal amefunga mabao saba katika mechi 25 alizocheza Bundesliga.


Mane alipamba vichwa vya habari kufuatia ugomvi kati yake na mchezaji mwenzake Leroy Sane na akasimamishwa kazi na kutozwa faini.


Mane aliulizwa na mtangazaji wa Senegal 2sTV kama ataendelea kukipiga Bayern, Mane. alisema:


“Ndiyo, Mungu akipenda. Endapo mambo yataenda sawa nitacheza Bayern, ninapenda changamoto kwahiyo nachopitia ni jambo la kawaida, Ulikuwa msimu mgumu sana.”



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz