Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Yanga U20 imekumbana na kipigo kisichotarajiwa cha bao 1-0 kutoka kwa Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya Vijana U20 iliyopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Pamoja na kutawala mchezo, vijana wa kocha Said Maulid "SMG" walikosa umakini katika lango la Dodoma Jiji
Unaweza kusema pengo la Clement Mzize ambaye alikuwa mfungaji bora msimu uliopita, halijazibwa
Mzize alipandishwa timu ya wakubwa, licha ya umri wake kuruhusu kushiriki michuano hiyo, amewapisha vijana wengine waonyeshe vipaji vyao
Yanga iliruhusu bao dakika za lala salama, sasa italazimika kushinda mechi mbili zilizobaki dhidi ya Tanzania Prisons na Polisi Tanzania ili kuwa na nafasi ya kutinga robo fainali
Post a Comment