Hatutakuwa wanyonge msimu ujao - Try Again

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Jana klabu ya Simba iliandika rekodi ya kusaini mkataba wa udhamini wa jezi kwa miaka miwili wenye thamani ya Tsh Bilioni 4 na kampuni ya Sandaland The Only One

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Salim Abdallah 'Try Again'alitumia nafasi hiyo kueleza mikakati ya Simba kuelekea msimu ujao

Baada ya Simba kukosa mataji kwa misimu miwili mfululizo, Try Again amesema unyonge huo hautakuwepo msimu ujao, wamejipanga kushinda kila mashindano watakayoshiriki

"Niwahakikishie Wanasimba, tutakuwa na Simba imara na bora zaidi pengine kuliko wakati mwingine wowote"

"Tunawaambia wapinzani wetu wajiandae, msimu ujao watalia sana, muhimu tunaitaka Bodi ya Ligi ihakikishe wanasimamia haki," alisema Try Again

Aidha Try Again alibainisha kuwa michakato ya usajili inaendelea, wakati watakapoanza kutangaza wachezaji, Wanasimba watafurahi

"Tunaleta wachezaji bora na wenye hadhi ya kucheza klabu ya Simba ambao tunaamini wataweza kutusaidia kutimiza malengo yetu katika mashindano ya ndani na yale ya CAF kwa kuanzia Super League na Ligi ya mabingwa"

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post