Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa Kocha wao mpya, Miguel Gamondi hajaja kwa Bahati mbaya na ni kocha Mkubwa mwenye Mafanikio makubwa.
Kamwe amesema kuwa, mchakato wa kumpata kocha huyo ulianza mapema baada ya Kocha Nabi kuonyesha nia ya kutotaka kuendelea na Yanga msimu ujao.
"Hadi kukubali kuitumikia yanga aliomba kupitia kwanza Ripoti ya Kocha Nabi alipoishia na Mapemdekezo yake ndani ya timu akalizishwa nayo.
“Kocha wetu mpya naomba niwatoe hofu ameshiriki aslimia 100% kwenye usajili wetu Wa msimu huu hivyo kila mchezaji atakeichezea Yangasc kocha kapitisha na sio kumpangia.
“Pia, kocha mpya huwa anamapendekezo yake hivyo mtegemee kuwa na mabadiliko kwenye benchi la Ufundi kocha anaweza akaja na Watu wake alisema Ali kamwe Afsa Habari Yanga,” amesema All.
Post a Comment