Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Uongozi wa Yanga umempa Gamondi nafasi ya kuja na watu watatu katika benchi lake la ufundi wakiwemo kocha wa mazoezi ya viungo, kocha wa makipa na mtaalamu wa kuchambua mikanda ya wapinzani
Nafasi hizo ziliachwa wazi baada ya kuondoka kwa aliyekuwa Kocha Mkuu Nasreddine Nabi ambaye alipendekeza ujio wa Milton Nienov aliyekuwa kocha wa makipa, Helmy Gueldich aliyekuwa kocha wa mazoezi ya viungo na Khalil Ben Youssef aliyekuwa akifanya kazi ya kuchambua ubora wa timu pinzani kupitia mikanda ya video
"Kama ambavyo kocha aliyepita alikuja na watu wake na yeye (Gamondi) tumempa hiyo nafasi ashauri watu wa kuja nao tunachotaka awalete watu ambao watafanya kazi pamoja kwa ushirikiano siyo tumletee kisha baadaye wakaanza kupishana," alisema Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe
Kamwe amesema kama Gamondi atawahitaji baadhi ya watu waliokuwemo katika benchi la ufundi lililopita basi watawaita mezani kwa ajili ya mazungumzo ya mikataba mipya
Hata hivyo inafahamika kuwa Helmy na Ben Youssef wako bega kwa bega na Nabi, itawezekana kuwapata kama Nabi hatakuwa amepata timu ya kufundisha wakati huu baada ya mpango wa kutua Kaizer Chiefs kukwama
Post a Comment