Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Imefahamika kuwa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans wameanza rasmi mazungumzo ya kumsajili kiungo fundi wa kutoka DR Congo na Klabu ya Al Hilal ya Sudan, Fabrice Ngoma ambaye tayari uongozi wake umeomba kuvunja mkataba wake ili kumpa nafasi ya kuondoka kama mchezaji huru.
Mastaa wa kimataifa wa Klabu ya Al Hilal wametimka Sudan kutokana na vita inayoendelea nchini humo na kusababisha ligi kusimama, halia mbayo imeendelea kuleta taharuki kwa wadau wa soka nchini humo, kwa kuhisi huenda timu zao zikashindwa kufanya vizuri katika MIchuano ya Kimataifa simu ujao.
Rais wa Young Africans Injinia Hersi Said ameweka wazi mipango ya usajili wa klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao ambapo amesema kuwa ripoti kutoka kwa benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Nassredine Nabi inahitaji kuongeza majembe mapya na kupunguza wachezaji wengine.
Taarifa ambazo zimepatikana jijini Dar es salaam kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza juu ya Young Africans kumtengea mkataba wa miaka miwili kiungo huyo huku mazungumzo yakiwa yanaendelea baina ya pande zote mbili.
Taarifa kutoka DR Congo zinaeleza juu ya Young Africans kuanza mazungumzo ya kumsajili Fabrice Ngoma ambapo tayari wameshawasilisha ofa ya mkataba wa miaka 2 kumpata kiungo huyo ambaye kupitia uongozi wake umeweka wazi kuhitaji kuondoka Sudan kutokana na hali ilivyo.
“Uongozi wa Al Hilal upo kwenye wakati mgumu sana hiyo ni kutokana na hali ilivyo kwa sasa ya kiusalama nchini Sudan kuwa na machafuko hivyo wachezaji wengi sana wameomba kuondoka akiwemo Fabrice Ngoma.
“Young Africans tayari wamewasilisha ofa yao ya kumtaka Fabrice Ngoma ikiwa na mkataba wa miaka 2, tayari mazungumzo yanaendelea baina ya Young Africans na uongozi wa Ngoma na Al Hilal hivyo dili linaweza kukamilika muda wowote,” kimesema chanzo hiko.
Kabla ya kutuwa Al Hilal kati kati ya msimu huu Fabrice Ngoma aliwahi kucheza katika klabu kadhaa za ndani na nje ya DR Congo ambazo ni FC Arc-en-Ciel – DR Congo (2013–2014), Sharks XI – DR Congo (2014–2015), MK Etanchéité – DR Congo (2015–2017), Ifeanyi Ubah – Nigeria (2017), AS Vita Club – DR Congo (2017–2019), Raja CA (2019–2022) na Al-Fahaheel SC – Kuwait (2022-2023).
Chanzo: Dar24
Post a Comment