Dirisha la maoni TPLB lafunguliwa rasmi

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imefungua rasmi dirisha la kupokea maoni ya maboresho ya kanuni za Ligi Kuu Bara, Ligi ya Championship na First League kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea msimu wa 2023/2024.


Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya bodi hiyo imesema wamefungua dirisha hilo kwa ajili ya kuandaa na kutengeneza kanuni zitakazotumika katika msimu ujao.


“Bodi imekuwa na utaratibu wa kukusanya maoni kutoka kwa wadau wa mpira wa miguu hususani ligi hizo tatu ili kupata mawazo mapya ya namna ya kuendelea kuboresha uendeshaji na usimamozi wa ligi,” imeeleza taarifa hiyo


Imewataka wadau ambazo ni pamoja na mashabiki, wanahabari, vyama vya mpira wa miguu, wadhamini, taasisi za kiserikali na binafsi kutuma maoni yao kupitia barua pepe Maoni@ligikuu.co.tz, kabla ya saa 5:59 usiku ifikapo Juni 30, mwaka huu.


Chanzo: Dar24

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post