Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Jana mshambuliaji wa Marumo Gallants Ranga Chivaviro kupitia 'Insta Live' aliwapa furaha Wananchi baada ya kujirekodi 'mbashara' akiwa amevaa jezi ya Yanga huku pia eneo alipo likionekana ni Tanzania
Chivaviro aliyemaliza nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) akifunga mabao sita nyuma na kinara Fiston Mayele aliyemaliza na mabao saba, anaweza kuwa mchezaji wa Yanga msimu ujao
Ni ahadi ya Rais wa Yanga aliyoitia wakati yuko Afrika Kusini kuwa msimu huu atashusha mchezaji mmoja kutoka ligi kuu ya Afrika Kusini
Chivaviro alishika nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji bora Ligi Kuu ya Afrika Kusini msimu uliomalizika alifunga mabao 10 na assist mbili
Peter Shalulile wa Mamelodi Sundowns na Khanyisa Mayo wa Cape Town City walimaliza wafungaji bora kila mmoja akifunga mabao 12
Post a Comment