Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Golikipa namba moja wa Simba SC, Aishi Manula, atakuwa nje kwa miezi minne baada ya kufanyiwa upasuaji wa nyama za paja.
Aishi alipata majeraha katika mechi ya robo fainali ya kombe la Azam Sports Federation dhidi ya Ihefu FC iliyochezwa Aprili 7, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.
Upasuaji huo alifanyiwa Mei 30, 2023 nchini Afrika Kusini ambapo kwa mujibu wa Simba APP, golikipa huyo namba moja wa Taifa Stars, atarejea kesho na kuendelea na sehemu ya pili ya mazoezi ya viungo ili aweze kupona vizuri.
"Atakuwa nje kwa takriban miezi minne akifanya mazoezi ya viungo ili jeraha lipone vizuri," alisema daktari wa timu Edwin Kagabo.
Post a Comment