Benzema asaini Al Ittihad

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA.


 Aliyekuwa mshambuliaji wa Klabu ya Real Madrid, Karim Benzema tayari ameshasaini mkataba wa awali na Klabu ya Al Ittihad ya Saudi Arabia.


Benzema ambaye ni raia wa Ufaransa tayari ameshaagwa na klabu yake ya Madrid, mkataba mkubwa anaotarajia kusaini na Ittihad utakuwa wa miaka miwili mpaka 2025.


Benzema ameitumikia Madrid kwa miaka 14 tangu 2009 akitokea Olympic Lyon ya Ufaransa na kupata mafanikio makubwa akiwa na miamba hao wa La Liga.


Akiwa na Madris, Benzema ameshinda mataji 25 ikiwemo UEFA Champions Leagues mara tano, La Liga mara nne na Copa del Rey mara tatu.


Pia ndiye mchezaji anayeshikiliza Tuzo ya Ballon d'Or ya mchezaji Bora wa DUnia wa mwaka. Pia, ni mfungaji bora wa pili wa muda wote wa Madrid 353 nyuma ya Cristiano Ronaldo mwenye mabao 450.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post