Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mlinda lango Beno Kakolanya amekiri kuwa magolikipa wengi hapa Tanzania (akiwemo yeye) wanapata ujuzi kutoka kwa mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra
Kakolanya anayetajwa kuwa mbioni kujiunga na Singida Fountain Gate Fc baada ya kuachana na Simba, amesema Diarra amepitia misingi yote ya ugolikipa kitu ambacho magolikipa wengi hapa nchini hawana
"Binafsi nafurahi kumuona Djigui Diarra kwenye ligi yetu, ni golikipa bora sana ambaye anatufunza vitu vingi sisi magolikipa wazawa kwa sababu yeye amepitia basics ya goal-keeping"
"Magolikipa wengi wa Tanzania tunaibukia mitaani, hatufundishwi tangu utotoni. Kwangu Diarra ni mwalimu," alisema Beno
Katika misimu miwili aliyoitumikia Yanga, Diarra ameshinda tuzo ya golikipa bora wa msimu msimu huu akiondoka na tuzo nyingine zaidi kipa bora wa michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika na kipa bora wa kombe la Shirikisho la Azam Fc
Post a Comment