Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mchezaji wa klabu ya soka ya Yanga Yannick Litombo Bangala amethibitisha kwamba bado anayo nafasi kubwa ya kuendelea kusalia kwenye kikosi hicho kwa msimu ujao kutokana na kuwa na mkataba na miamba hiyo ya soka hapa nchini.
Mbali na hayo, Bangala amesema kwamba anajisikia fahari kwasababu amekuwa ni mmoja kati ya wachezaji ambao wameweza kuisaidia timu yake kufika hatua ya fainali katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika huku akisisitiza kwamba bado anatamani kuendelea kusalia hapa nchini kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo kwa nchi ya Tanzania.
Bangala ameyasema hayo alipohojiwa na kituo kimoja cha habari hapa nchini alipoulizwa kuhusu kuondoka kwake kwenye timu ya wananchi kama jinsi ambavyo tetesi mbalimbali zimekuwa zikisikika kwamba huenda kiungo huyo akaachana na waajiri wake, timu ya wananchi, Yanga.
Post a Comment