Baada ya kumnyakua Fei toto, Azam sasa wahamia kwa Simba SC

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Baada ya kumalizana na Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ akitokea Young Africans, Uongozi wa Azam FC unatajwa kuhamishia nguvu Simba SC ukijipanga kumsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Malawi Peter Banda.


Taarifa zinaeleza kuwa Azam FC imeanza mazungumzo na wawakilishi wa nyota huyo wa kimataifa wa Malawi mwenye miaka 22.


Inaelezwa kwamba kwa hatua waliyofikia kuna uwezekano mkubwa Banda akavaa uzi wa Azam FC msimu ujao kutokana na Simba SC kuwa tayari kumuuza au kumtoa kwa mkopo kipindi hiki akiwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja.


Nyota huyo tegemeo wa timu ya taifa ya Malawi hayupo kwenye mipango ya kocha mkuu, Roberto Oliveira Robertinho’ aliyowapa mabosi wa chama hilo na Azam inatumia mwanya huo ili kumshawishi atue Chamazi yalipo maskani yao.


Mmoja wa viongozi wa juu wa Azam FC mesema: “Pale Simba tutang’oa mtu kama tulivyowapa wao wachezaji miaka ya nyuma na sisi watatupa mastaa wao mmoja wao ni yule winga Banda. Kama wanaona hawafai, sisi atatufaa na tunajua tutamtumiaje” amesema mtu huyo.


Banda alisajiliwa Simba SC mwanzo a msimu uliopita akitokea Nyassa Big Bullets ya Malawi, lakini tangu ametua hana mwendelezo huku majeraha ya mara kwa mara yakitajwa kumtesa Juhudi za kumpata Banda kuzungumzia suala hilo wala viongozi wa Simba jana harikuzaa matunda.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post