Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Azam Fc ni kama wameweka kambi Jangwani, kwani baada ya kumn'goa Feisal Salum 'Fei Toto', timu hiyo inahusishwa kumuwania kiraka Yannick Bangala
Baada ya mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Azam Fc dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Mkwakwani Juni 12 na Yanga kutwaa taji hilo kwa ushindi wa bao 1-0, camera za Azam TV zilimnasa Mtendaji wa Azam Fc Abdulkarim Popat akifanya mazungumzo na wachezaji wawili wa Yanga, Bangala na Bernard Morrison
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alibaini tukio hilo na kwenda kuwaondoa wachezaji wake akionekana kutofurahishwa na mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea
Bangala ameonekana katika kipande cha video kilichosambaa mitandaoni akidai ana asilimia 20 za kubaki Yanga na asilimia 80 za kuondoka licha ya kuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Yanga
Meneja wa Bangala alikiri kuwa mteja wake bado ana mkataba na Yanga lakini hawana uhakika kama ataendelea kubaki Jangwani
Kwa upande mwingine ni kama Bangala hana furaha baada ya kupoteza nafasi katika kikosi cha kwanza cha Yanga
Msimu uliomalizika haukuwa mzuri kwake, aliyekuwa Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi alimuondoa katika nafasi ya beki huku akikosa uhakika wa kucheza katika eneo la kiungo mbele ya Mudathir Yahya, Salum Abubakar 'Sure Boy' na Khalid Aucho
Post a Comment