Azam FC watambulisha Mshambuliaji toka Raja Casablanca ya Morocco

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Azam FC imeanza kushusha vifaa kwa ajili ya msimu ujao baada ya kupitisha fagio la wachezaji ambao hawataendelea nao.


Leo Azam imeanza kwa kutambulisha mshambuliaji aliyenunuliwa kutoka klabu ya Raja Casablanca, Djirril Sillah.


Kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii wameandika; "Tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumefikia makubaliano na klabu ya Raja Casablanca, ya kumnunua kiungo wao mshambuliaji, Sillah,"


Nyota huyo wa Gambia, anatarajia kutua nchini muda wowote kuanzia sasa kumalizia taratibu za mwisho za usajili.


Msimu uliopita kwenye Ligi Kuu ya Morocco, Sillah alifanikiwa kufunga jumla ya mabao saba na kutoa pasi za mwisho nne, wakati akiwa kwa mkopo JS Soualem.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post