Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kiungo wa kimataifa anayekipiga klabu ya Yanga, Khalid Aucho ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka nchini Uganda inayotolewa na mtandao wa Pulse Sports wa nchini humo.
Aucho kwenye tuzo hiyo amewashinda mlinda mlango wa Mamelodi Sundowns Dennis Onyango na nyota wa Vipers SC, Yunus Sentamu.
"Ni heshima kupokea tuzo hii, ni ushahidi kwamba bidii yangu inaonekana na kutambuliwa," amesema Aucho
"Kwa kweli napenda kuwashukuru mashabiki wangu wa Uganda na Yanga kwa kunipigia kura mchezaji bora, niwaahidi kuwalipa kwa kazi zaidi,"
"Mwaka jana, kama timu tulifanya kazi kwa bidii na kushinda mengi. Tumefanya vivyo hivyo na ninaweza kushinda tuzo hiyo tena," ameongeza Aucho
Aucho amekuwa na mafanikio makubwa 2022 akiwa na Yanga ambapo ameiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/23, Ngao ya Jamii na Kombe la Azam Shirikisho na kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ikishika nafasi ya pili.
Hapo awali, tuzo hiyo ilishinda Allan Okello mwaka 2019, Nicholas Wadada 2020 na Taddeo Lwanga 2021.
Chanzo: Mwanaspoti
Post a Comment