Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema baada ya watani Yanga kucheza fainali ya kombe la Shirikisho sasa hakuna kichaka cha kujificha, Simba inahitaji kuweka rekodi kubwa zaidi ambayo ni kutwaa ligi ya mabingwa
Ahmed amesema Yanga imewachukua miaka 30 kuvunja rekodi ya Simba kucheza fainali ya mashindano ya CAF licha ya udogo wa mashindano waliyoshiriki
Amesema mashabiki wa Simba sio wa kukaa mpaka usiku kusubiri mchezo wa watani zao huku furaha yao ikiwa watani kukosa ubingwa
Ahmed amesema Simba imeweka historia kwa kufanya vizuri katika mashindano makubwa ya CAF wakizifunga timu zote kubwa barani Afrika, hivyo sasa hawana sababu ya kusema hawawezi kushinda ubingwa wa Afrika
Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Ahmed ameandika ujumbe huu;
UTO kakosa kombe tumefurahi na ukweli hatuwezi kujificha tumefurahi sana
Lakini hii sio aina ya furaha tunayoitaka wana Lunyasi
Sisi tunataka furaha yetu ya kutwaa wa Ubingwa wa Afrika
Ni fedheha kubwa sisi kukaa macho usiku kuangalia UTO anacheza fainali
Pamoja na ukweli kwamba njia yao ilikua nyepesi lakini ukweli mwingine ni kwamba wamejua kuitumia iyo njia ya nyepesi
Sisi hua tunapita njia ngumu ni wakati wa kutafuta namna ya kupita kwenye iyo njia ngumu haiwezi kuwa excuse tena eti tumepita njia ngumu
Tumeshamfunga Al Ahly, tushamfunga Wydad nani mwingine mkubwa kabaki jibu ni hakuna kama hakuna kwanini tusichukue huu ubingwa
Imewachukua UTO miaka 30 kufikia rekodi yetu ya kucheza Fainali ya CAF, Sasa tunapaswa kuweka rekodi mpya Afrika
Tunapaswa kuamka ili tuwe wa kwanza kuweka rekodi mpya ambayo UTO atahangaika kuifikia
Kazi kubwa inatakiwa kufanyika ndani na nje ya Uwanja tena ianze sasa
Tunahitaji wachezaji wenye hadhi ya kutupa ubingwa wa Afrika, hadhi ni pamoja na ubora na kujitoa kwa ajili ya timu yetu
Post a Comment