Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kupitia Instagram Ahmed amewapongeza waliotwaa ubingwa na waliopata tuzo na wasimamizi wa Ligi pamoja na waaandaji wa tuzo.
"Kwetu Simba tuwapongeze nyota wetu waliotwaa tuzo hakika wametuheshimisha. Kiujumla kama timu hatuna cha kujivunia sana maana hatujapata tulichokihitaji msimu huu," ameandika Ahmed na kuongeza
"Hii inatupa nafasi ya kujipanga zaidi kwa msimu ujao. Ubingwa unahitaji wachezaji bora na timu imara. Ni jukumu letu viongozi kutafuta wachezaji sahihi na kutengeneza timu madhubuti, na hilo limeshaanza kufanyika kwa umaridadi wa hali ya juu sana," ameandika Ahmed
Meneja huyo ameeleza kiu na shauku kubwa ya Wanasimba ni kuona mataji yanarejea kwenye timu yao kwani wamechoka kelele za jirani
"Timu kubwa kama Simba haipaswi kukaa muda mrefu bila mataji, miaka miwili inatosha ni muda sasa wa kurudisha ufalme na wetu. Tukutane 2023/2024,"
Chanzo: Mwanaspoti
Post a Comment