Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Simba jana Juni 6 ilishinda mabao 6-1 huku Saido akiweka wavuni mabao 5 akipaa kutoka 10 hadi 15.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wanakitaka kiatu cha ufungaji bora msimu wa 2022/23 na mechi ya mwisho ya msimu watamsaidia Saido ili akibebe.
Ligi Kuu Bara imebaki mechi moja kutamatakika ambapo Simba itacheza dhidi ya Coastal Union Dar na Yanga itacheza dhidi ya Tanzania Prisons Sumbawanga.
"Tunahitaji mfungaji bora, zimesalia bao 2 na hakuna mashaka kwenye mechi ya mwisho ya Coastal tutamsaidia timu nzima awe mfungaji bora," amesema Ahmed na kuongeza;
"Uliona kuna nafasi John Bocco alikuwa nafasi ya kufunga akasema hii ya Saido akamwekea akafunga, bao la tano alikuwa na uwezo wa kufunga Kibu lakini akamtengea Saido,"
Chanzo: Mwanaspoti
Post a Comment