Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
USM Alger wametoa malalamiko kupitia ukurasa wao wa Instagram kusema kuwa wenyeji wao waliwapulizia dawa kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo kwa sababu kilikuwa na harufu mbaya ambayo iliwaathiri baadhi ya maafisa wao, lakini walipohitaji msaada hawakupata huduma stahiki kama wageni wa mchezo.
“Tuna shutumu vikali unyanyasaji wa kupuliziwa dawa katika chumba cha kubadilisha nguo katika Uwanja wa Mkapa, baada ya uongozi wetu kupokea taarifa hizo kufanyiwa unyanyasaji, walituma mjumbe kufuatilia mambo kabla ya wajumbe hao kufika.
“Kwa bahati nzuri kwa timu yetu, Kiongozi wetu alipogundua jambo hilo kabla ya wachezaji kufika uwanjani, aliwasilisha malalamiko kwa wawakilishi wa CAF waliokuwepo uwanjani kuona hali iliyokuwepo, nao waliandika ripoti kuhusu tukio hilo” ni sehemu ya ujumbe wa USMA uliotafsiriwa kutoka katika lugha ya kiarabu
Hata hivyo bado Shirikisho la Soka Barani ‘CAF’ Afrika halijathibitisha kupokea taarifa za malalamiko hayo kutoka USM Alger, na kama itathibitika kuna ukweli wa jambo hilo, huenda Young Africans ikashukiwa na adhabu ya kutozwa faini.
Timu hizo zitakutana tena Jumamosi (Juni 03) katika Uwanja wa du 5 Juillet nchini Algeria, huku Young Africans ikihitajika kusaka ushindi wa mabao 2-0 ama zaidi ili kujihakikishia Ubingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, lakini USM Alger watahitaji sare ama ushindi wowote ili kufanikisha azma ya kutawazwa kuwa mabingwa msimu huu 2022/23.
Chanzo: Dar24
Post a Comment