Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema uongozi wake umeendelea kutimiza wajibu wake kwa mchezaji Feisal Salum licha ya kuwa hayuko na timu kwa takribani miezi sita sasa
Hersi amesema Yanga imeendelea kumlipa mshahara mchezaji huyo huku akibainisha kuwa wamempa machaguo matatu ambayo yataweza kuhitimisha mgogoro uliopo
"Feisal bado anaendelea kupokea Mshaharaa Yanga, amepokea hadi mwezi January, lakini baada ya hapo akaunti yake ilianza kuwa na shida kwa kuwa inarejesha pesa ila kila mwezi tunamuingizia pesa lakini zinarudishwa na ushahidi tunao, tumeomba akaunti mbadala ili tumuwekee pesa zake, atakapo tupa akaunti hiyo sisi tutamuingizia pesa zake zote"
"Lakini pia tumempa machaguo matatu ambayo anaweza kuyafuata ili kumaliza hii sintofahamu; Moja arudi kutumikia mkataba wake ambao utamalizika May 2024. Pili kama tatizo ni maslahi tumemwambia aje tuzungumze kwasababu upande wa Yanga hatuna shida na kumboreshea maslahi yake. Tatu kama kuna klabu inayomtaka Feisal ije tuzungumze nayo sisi kama Yanga wala hatuna shida," alisema Hersi
Aidha Hersi amesema anaamini kuna jambo liko nyuma ya mogogoro uliopo kwani katika wakati wote ambao Feisal ameitumikia Yanga hakuwahi kuwa mtovu wa nidhamu
"Feisal ni mmoja kati ya Wachezaji bora na wenye nidhamu ambao tumewahi kuwa nao Yanga hadi leo. Katika Wachezaji ambao niliwakuta Yanga, yeye ni mchezaji mkongwe zaidi kati ya wote sababu hakuna yeyote aliyesalia Yanga hadi leo ispokuwa yeye"
"Lakini pia hajawahi kuwa na changamoto yoyote ya kinidhamu, alikuja akiwa mdogo ndio maana akapewa jina la Fei Toto. Kama GSM tuliwahi kumwita Feisal na kukaa nae kujadili maslahi yake ambayo hayakuwa madogo hata kwa wakati huo, alikuwa akipokea mshahara wa Tsh 1.5m na tukamuongezea hadi kufikia Tsh Million 4 kwa mwezi pamoja na fedha ya usajili ya Tsh Million 100"
"Kuna Watu wanauliza kuhusu maslahi ya Feisal ikiwa sisi tuliyaboresha tangu mwaka 2020. Sitaki kwenda mbali ila mimi naamini kuna kitu nyuma ya Feisal kinachomsukuma kufanya haya"
Post a Comment