Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa kwa kushirikiana na wachekeshaji nchini wameandaa ‘Wananchi Comedy Festival’ kwa ajili ya kuwacheka wote waliokufa kiume (kushindwa kuingia nusu fainali) wakiwemo watani wao Simba.
Akizungumza leo Mei Mosi kwenye makao makuu ya klabu yaliyopo Jangwani wamesema tamasha hilo litafanyika Mei 5, 2023 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere International Conversation Centre ambalo itakuwa ni Stand Up Comedy waliopita jina la “Wananchi Comedy Festival”.
“Tumefurahi na lazima tukaonyeshe furaha yetu, kwa hiyo tumeandaa WANANCHI COMEDY FESTIVAL, NJOONI TUWACHEKE wote Waliokufa kiume, kilele chao cha kuchekwa kitakuwa ni Mei 05, 2023, mashujaa wote waliokufa kiume Afrika nzima kilele chao cha kuchekwa ni Tar 05.
“Ukiona ulikufa kiume, hujaua wanaume Tarehe 5 una shughuli ya kuchekwa na Yanga, Hii ni siku ya wanachama, washabiki wa Yanga tunakutana mahali tucheke tufurahi,” Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe
Show hiyo itakuwa na wacheleshaji nguli wa stand up comedy kama Ndalo, Coy Mzungu na TX Dullah “Tumefurahi na lazima tukaoneshe furaha yetu, tumeandaa Wananchi Comedy Festival njoeni tuwacheke waliokufa kiume,” amesema Ally Kamwe.
Post a Comment