Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Vinara wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga jioni ya leo watashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi kupepetana na Dodoma Jiji katika mchezo ambao Wananchi wana nafasi ya kutwaa ubingwa kama wataibuka na ushindi
Wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 71, alama nne zaidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili, Yanga inahitaji alama tatu tu kutwaa ubingwa
Simba imesalia na mechi mbili ambazo wakishinda zote watafikisha alama 73, ushindi kwa Yanga leo utawafanya wafikishe alama 74
Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi kwani hata Dodoma Jiji wanahitaji matokeo mazuri ili kujihakikishia usalama wa kubaki ligi kuu msimu huu
Lakini ubora wa kikosi cha kocha Nasreddine Nabi unawapa nafasi zaidi Yanga kushinda mchezo huo na kujihakikishia ubingwa kabla ya kusafiri Afrika Kusini wanakokabiliwa na mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants. Yanga itaondoka nchini Alfajiri ya kesho Jumapili kuelekea Afrika Kusini
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema shamrashamra kuelekea mchezo huo zitaanza saa sita mchana ambapo kutakuwa na burudani za utangulizi kuelekea muda wa mchezo ambao ni saa 10 jioni
Post a Comment