Yacouba, Makambo kupewa mikataba minono

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Klabu ya Kitayosce FC (Tabora united) imwedhamiria kumsajili Mshambuliaji wa Ihefu FC Yacouba Sogne pamoja na Mshambuliaji wa zamani wa Young Africans Herietier Makambo ili kuboresha kikosi cha klabu hiyo ambayo itashiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2023/24




Aidha, Kitayosce pia wameonyesha nia ya kuipata huduma ya Mlinzi wa kati wa klab ya Kagera Sugar raia wa Ghana Steven Duah


Kitayosce FC itashiriki Ligi Kuu msimu ujao ikitokea Ligi ya Championship sambamba na Mabingwa wa ligi hiyo JKT Tanzania, na sasa imeanza kujipanga kufanya usajili wa wachezaji wenye uzoefu na Mshike Mshike wa michuano hiyo mikubwa nchini Tanzania


Katibu Mkuu wa timu hiyo, Adam Simba amesema wanataka kuwasajili Yacouba Sogne, Steven Duah na Herietier Makambo ambao anaamini kuwa watawasaidia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao wa mwaka 2023/24


"Kuhusu wachezaji hao, bado hatujasainiana nao mikataba Kwakuwa tunasubiri michezo ya Ligi Kuu imalizike na dirisha la usajili lifunguliwe tukamilishe usajili wao"


"Ukiachana na wachezaji hao tutasajili wachezaji wengine wakubwa wa ndani na nje ya nchi lengo letu likiwa ni kuhakikisha tunakuwa washindani wa Ligi Kuu msimu ujao na sio washiriki," amesema Simba

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post