Katika kuonesha mshikamano kwa winga Vinicius Jr kufuatia sakata lake la ubaguzi wa rangi, wachezaji wa Real Madrid waliingia uwanjani wakiwa wamevalia jezi namba 20 ya Vinicius Jr kabla ya mchezo wao wa leo dhidi ya Rayo Vallecano.
Naye Vinicius Jr ambaye hakuwa sehemu ya kikosi kinachoanza kutokana na majeraha alijitokeza na kuwashukuru watu wote kwa upendo na mshikamano alioupata.
Aidha kulikuwa na bango kubwa lililopeperushwa uwanjani hapo lenye ujumbe “SISI SOTE NI VINICIUS, IMETOSHA SASA BASI” huku wachezaji wa timu zote mbili pia wakipiga picha na bango lililokuwa na ujumbe, "Wabaguzi wa rangi, hawatakiwi kwenye soka."
Mnamo dakika ya 20 ya mashabiki pia walimpigia makofi ya shangwe (standing ovation) mchezaji huyo ambaye naye alijitokeza uwanjani na kuwashukuru
Post a Comment