Utatu huu Simba ni balaa zito

 

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Utatu wa nyota watatu ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira una balaa kutokana na kasi yao kwenye kufunga na kutengeneza nafasi za mabao.


Ipo wazi kuwa Yanga ni mabingwa wakiwa na pointi 74 kibindoni na kinara wa utupiaji ni Fiston Mayele mwenye mabao 16.


Nyota Mayele amekuwa kwenye ubora ndani ya Yanga katika kutimiza majukumu yake ametoa pasi mbili za mabao.


Ni Jean Baleke amekuwa mwiba baada ya kujiunga na timu hiyo kwenye dirisha dogo akiwa amefunga jumla ya mabao 8 kwenye ligi.


Mshikaji wake Saido Ntibanzokiza yeye kafunga mabao sita akiwa na uzi wa Simba huku yale manne akifunga alipokuwa ndani ya Geita Gold na ametoa pasi sita za mabao akiwa na Simba na sita alitoa akiwa ndani ya Geita Gold.


Jumla Saido kafunga mabao 10 kwenye ligi na pasi za mabao ni 12 akiwa ni namba mbili kwa mastaa wenye pasi nyingi msimu wa 2022/23.


Mwamba mwingine ni Clatous Chama ambaye ni namba moja kwa watengeeza pasi za mwisho akiwa amefunga mabao manne na ametoa pasi 14 za mabao.


Viungo wawili Chama na Ntibanzokiza wamekuwa na balaa kwenye mapigo huru ambapo kwenye mchezo dhidi ya Namungo, alitoa pasi iliyotumiwa na Baleke katika mchezo wa ligi na Chama kwenye pasi zake 14 mchezo dhidi ya Singida Big Stars alitoa pasi mbili.


Katika pasi zake mbili ambazo alitoa kwa mapigo huru moja alimpa mshikaji wake Ntibanzokiza na kuongeza nguvu kwenye utatu wenye ushikaji wa kucheka na nyavu.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post