Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA.
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Namungo Fc imewavurugia hesabu katika mbio za ubingwa
Ahmed amesema walihitaji kushinda mchezo huo ili kupunguza gap la pointi dhidi ya timu inayoongoza ligi lakini sasa ni wazi nafasi imekuwa finyu
"Tulishinda mechi iliyopita dhidi ya anayeongoza ligi, tulipaswa kushinda leo (jana) ili kuzidi kupunguza gap lakini tumedondosha alama mbili. Ikitokea mpinzani wetu ameshinda mchezo wake unaofuata maana yake gap litaongezeka zaidi"
"Kwa kuangalia mechi zilizobaki kwa kweli ni haki kila mmoja kuchukua upande wake, kuna waliokata tamaa ya ubingwa kwa sababu ki uhalisia nafasi yetu ni ndogo lakini kuna wenye imani ya kuendelea kupambana wakiamini lolote linaweza kutokea," alisema Ahmed
Aidha akizungumzia mabadiliko ya kikosi yaliyofanywa na kocha Robertinho Oliveira, Ahmed amesema ipo tahadhari ilichukuliwa kwa baadhi ya wachezaji waliokuwa na kadi mbili za njano
"Kuna wachezaji walikuwa na kadi mbili za njano, tusisahau tuna mchezo wa nusu fainali ya kombe FA dhidi ya Azam Fc. Hivyo yapo mabadiliko ambayo yalilenga mchezo huo kwa kuwa tunahitaji kushinda na kutinga fainali"
Post a Comment