Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kikosi cha Yanga kiliwasili mkoani Singida jana na jioni kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida BS ambao utapigwa Alhamisi, May 04 katika uwanja wa LITI
Meneja wa timu hiyo Walter Harrison amesema wametua Singida wakiwa na dhamira moja tu, kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo
Yanga inaongoza Ligi ikiwa na alama 68, alama tano zaidi ya wapinzani wao Simba wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na alama 63
Leo Simba inachuana na Namungo Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Majaliwa ambapo kama Simba watafanikiwa kuondoka na alama zote tatu watapunguza gap la pointi kutoka tano na kuwa mbili na kusalia mechi tatu
Lakini kama Yanga itashinda dhidi ya Singida BS itarejesha alama tano kileleni huku zikisalia mechi tatu za kuhitimisha msimu ambayo Wananchi watahitaji alama nyingine tano kutoka kwenye mechi hizo ili kuwa mabingwa
"Kikosi kimewasili salama Singida, jioni wachezaji walipata nafasi ya kufanya mazoezi ya kwanza hapa. Tutakamilisha mazoezi yetu ya mwisho kesho (leo) katika uwanja wa LITI"
"Tumekuja hapa kusaka ushindi ili tujiweke katika nafasi nzuri ya kutetea taji letu. Tunafahamu mechi hizi za mwishoni mwa msimu ni ngumu lakini tumekuja hapa kupambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri," alisema Walter
Baada ya mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA kusogezwa mbele, Yanga itarejea jijini Dar es salaam baada ya mechi dhidi ya Singida BS ili kujiandaa na mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya Malumo Galants ambao utapigwa Jumatano ijayo, May 10 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Post a Comment