Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Yanga imeiwakilisha vyema Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika ikiwa moja ya timu nne zilizotinga nusu fainali ya michuano hiyo
Suluhu na bila kufungana dhidi ya Rivers United jana imewavusha Wananchi kwenda nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-0 waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Nigeria
Yanga imeungana na Asec Mimosas iliyopata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya US Monastir pamoja na Malumo Galants ya Afrikca Kusini iliyopata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Pyramids ya Misri
Timu ya nne kutinga nusu fainali ni USM Alger ambayo licha ya kufungwa mabao 3-2 na US FAR ya Morocco, imefuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-4
Katika hatua ya nusu fainali, Yanga itachuana na Malumo Galants wakati Asec Mimosas itachuana na USM Alger
Mechi za nusu fainali zitappigwa May 10 na May 17, Yanga na Asec zikianzia mechi zao nyumbani
Post a Comment