Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Liverpool wanataka kumsajili kiungo Khephren Thuram msimu huu wa joto.
Mazungumzo yameanza kujaribu kumsajili lakini kunaweza kuwa na ugumu kwa sababu klabu ya OGC Nice hawataki kumuuza.
Chanzo: [L'EQUIPE]
Karim Benzema amefanya uamuzi wake wa juu ya mustakabali na Real Madrid tayari wanajua.
Chanzo: [The Athletic]
Tottenham Hotspur watadai karibu euro million €100m kwa Harry Kane kwa klabu ambayo inatoka nje ya England, na watadai kiasi cha euro million €150 kwa klabu ya EPL ambayo itahitaji huduma ya mshambuliaji wake.
Chanzo: [tw/La_SER]
Neymar Jr hajioni popote zaidi ya PSG-Paris Saint-Germain au Manchester United katika msimu ujao.
Amekataa ofa ya mkataba kutoka huko Saudi Arabia.
Chanzo: [Foot Mercato]
Liverpool wameaza mazungumzo ya uhamisho na wawakilishi wa Manu Kone.
Kiungo huyo wa kati wa Borussia Monchengladbach mwenye umri wa miaka 22 yuko juu kwenye Orodha yao.
Chanzo: [SPORT BILD]
Saudi Arabia inamtaka Leo Messi na Karim Benzema.
Mkataba wenye thamani ya euro million €400 wa miaka 2 unamsubili Karim Benzema na mwingine kama balozi wa Kombe la Dunia 2030.
Chanzo: [Diario AS]
Bayern Munich wako tayari kulipa ada ya euro million €100 kwa West Ham United kwa ajili ya Declan Rice.
Tayari Thomas Tuchel amekwisha kuzungumza kwa njia ya simu kuhusu kuungana naye huko Bayern.
Chanzo: [Florian Plettenberg]
Bernado Silva ndiye plani B ya Barcelona ikiwa watashindwa kumsajili Leo Messi msimu huu wa kiangazi.
Chanzo: [Gerard Romero]
PSG-Paris Saint-Germain wanataka kumsajili kiungo wa klabu ya Arsenal Martin Odegaard, hata hivyo kiungo huyo ni sehemu muhimu ya mipango ya Mikel Arteta katika kusonga mbele hatua yoyote haitawezekana.
Chanzo: [Daily Mail Sport]
Real Madrid itamfanya Harry Kane kuwa kipaumbele katika usajili wa mshambuliaji ikiwa Karim Benzema ataondoka klabuni hapo.
Chanzo: [tw/COPE]
Real Madrid wanajiandaa kumsajili mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Stoke City na Newcastle United Joselu kwa mkataba wa mkopo wa mwaka 1 bure.
Chanzo: [MARCA]
Jude Bellingham atatangazwa kama mchezaji mpya wa Real Madrid huko Santiago Bernabeu kama katika wiki mbili zijazo.
Chanzo: [Diario AS]
Chelsea wametoa ofa ya euro million €60m pamoja na nyongeza ya €5m, huku David Fofana akijumuishwa kwa mkopo ili kupata saini ya Manuel Ugarte kutoka Sporting.
Kiungo huyo angependele kujiunga na klabu ya Chelsea kuliko PSG.
Chanzo: [Record Portugal]
Kambi ya Leo Messi tayari imekubali ofa kutoka katika Klabu ya Al Hilal yenye thamani ya euro billion €1.2 (kwa mwaka €600m) kwa mkataba wa miaka 2.
Hiyo ni zaidi ya mara mbili ya kile Cristiano Ronaldo anapata
Chanzo: [Foot Mercato]
Benjamin Pavard anataka kuondoka Bayern Munich msimu huu wa kiangazi.
Hataongeza mkataba mpya na mkataba wa sasa unafikia tamati June 2024.
Chanzo: [Florian Plettenberg]
Tottenham Hotspur wameazimia kupinga majaribio ya Manchester United kumsajili mshambuliaji wao Harry Kane msimu huu wa kiangazi.
Dan Levy hataki kumuuza Kane katika Klabu ya pinzani ya EPL.
Chanzo: [Daily Mirror]
Juventus wanaongoza katika mbio za kuwania kumsajili winga wa klabu ya Chelsea Christian Pulisic.
Chanzo: [ESPN FC]
Saudi Arabia inamtaka Leo Messi na Karim Benzema.
Mkataba wenye thamani ya euro million €400 wa miaka 2 unamsubili Karim Benzema na mwingine kama balozi wa Kombe la Dunia 2030.
Chanzo: [Diario AS]
Bayern Munich wako tayari kulipa ada ya euro million €100 kwa West Ham United kwa ajili ya Declan Rice.
Tayari Thomas Tuchel amekwisha kuzungumza kwa njia ya simu kuhusu kuungana naye huko Bayern.
Chanzo: [Florian Plettenberg]
Post a Comment