Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Taarifa za ndani kutoka Simba zinaeleza kuwa beki wa kati wa klabu hiyo, Joash Onyango Achieng (30) amewasilisha kuomba kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.
Inadaiwa kuwa, sababu kubwa ya kutaka kuondoka ni kutokana na kuchoka kuandamwa na maneno ya mashabiki wa Simba na wachambuzi wa soka nchini kila timu hiyo inapopata matokeo mabaya na kwamba anahitaji kwenda kutafuta changamoto nyingine nje ya klabu hiyo.
Aidha, imedaiwa kuwa upo uwezekano asimalizie hata Michezo iliyosalia ya Ligi kuu na ambapo hadi sasa uongozi wa Simba bado haujampa majibu ya kumruhusu ama kumkatalia.
Onyango alijiunga na Simba Agosti 2020 kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Gor Mahia ya nyumbani kwao nchini kenya.
Aidha, Juni 2022 baada ya mkataba wake kumalizika, Onyango aliongeza mkataba mwingine mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia klabuni hapo mpaka mwakani 2024.
Ikumbukwe kuwa, mwanzoni mwa msimu huu, baada ya ujio wa beki wa kati kutoka Burkina Faso, Mohamed Ouattara ndani ya Simba na Onyango kuanza kupigwa benchi na Kocha Zoran Maki kiasi cha kukosa mechi mbili za awali za Ligi Kuu Bara sambamba na ile ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, beki huyo aliomba kuondoka klabuni hapo.
Wachezaji wengine wanaotajwa kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu ni; Nelson Okwa, Victor Akpan, Augustine Okrah, Mohamed Ouattara, Ismail Sawadogo, Gadiel Maichael, Mohammed Mussa, Beno Kakolanya, Peter Banda
Post a Comment