Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Biashara asubuhi, ndio maneno ya mabosi wa Simba ambao timu yao imeshindwa kufikia malengo msimu huu kwa kuanza mchakato wa usajili wa wachezaji wapya mapema lakini pia wakiweka wazi straika, Moses Phiri, haondoki.
Taarifa kutoka Simba zinasema tayari mazungumzo na baadhi ya wachezaji akiwamo winga, Martin Kiiza, golikipa Alfred Mudekereza wote wa Vipers ya Uganda na Sospeter Bajana wa Azam FC yameshaanza.
Mudekereza anapewa nafasi ya kumrithi kipa, Aishi Manula, ambaye huenda akapoteza namba yake katika kikosi cha Simba msimu ujao.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, aliliambia Nipashe jana wameshaanza mchakato wa usajili kwa lengo la kuboresha kikosi chake ili kiwe cha 'kutisha' katika msimu ujao na kurejesha ubabe wake.
Ahmed alisema wanasubiri ripoti rasmi ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira 'Robertinho' baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Bara lakini akiweka wazi Mzambia Phiri ataendelea kubakia klabuni hapo na si kweli ameandika barua ya kutaka kuondoka.
"Tunakisuka kikosi chetu, tunafanya maboresho pale ambapo panahitajika kufanya kwa ajili ya msimu ujao, ninavyokwambia wataalamu wetu wametawanyika sehemu mbalimbali Afrika na dunia kuangalia nani aingie kwa ajili ya kukiimarisha kikosi.
Maeneo gani yanatakiwa kuongezewa nguvu na nini tufanye kwa ajili ya kushinda makombe, baada hapo sasa tunashusha wale ambao tayari tumeshakubaliana nao," alisema Ahmed.
Aliongeza Phiri alishindwa kuhimili mikiki mikiki kutokana na majeraha aliyopata na hivyo mwalimu akawa anampa muda kidogo wa kucheza kwa ajili ya kutafuta utimamu wa mwili, sasa anaendelea kuimarika na msimu ujao anatarajiwa kurejea akiwa fiti zaidi.
Amewataka wanachama na mashabiki wa Simba kutohofia na wajipange kuona timu yenye ubora mkubwa katika msimu ujao baada ya kumaliza msimu wa pili mfululizo bila ya kutwaa kombe lolote, lakini pia ikiishia hatua ya robo fainali katika mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Post a Comment