TASWA yaipongeza Young Africans

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimeipongeza klabu ya Young Africans kwa kufanikiwa kuingia Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF Confederation Cup).


Young Africans imefuzu hatua hiyo baada ya kushinda mabao 1-2 katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya Nusu Fainali ya michuano hiyo uliofanyika jana huko Afrika Kusini.


Ushindi huo unafanya Young Africans ifuzu kwa jumla ya mabao 4-1, kwani katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, Tanzania wiki iliyopita Young Africans ilishinda mabao 2-0.


Taarifa ya TASWA iliyosainiwa na Katibu Mkuu Alfred Lucas imeeleza: TASWA tunaona fahari kwa mafanikio ya timu ya Tanzania kufikia hatua hiyo, hasa tukivuta kumbukumbu ya hatua kama hiyo iliyofanywa na Simba miaka 30 iliyopita pale ilipofuzu fainali ya mashindano ya Kombe la CAF.


Tunasema hongera sana kwa Yanga kwa kuiheshimisha nchi na kuitikia wito wa hamasa ya Rais wa Tanzanua Samia Suluhu Hassan, ambaye tangu hatua za mwanzo za michuano hii alionesha kuwa karibu na timu zote zilizoshiriki michuano ya kimataifa.


Tunaamini Yanga haitabweteka au kuridhika na kutinga fainali, badala yake itajipanga vizuri kwa michezo miwili ya fainali dhidi ya USM Alger na ilivyojipanga na kushinda michezo yote miwili ya Nusu Fainali.


Tunawaombea kila la heri wanetu, tunaomba Watanzania wote bila kujali itikadi zetu kushirikiana na Yanga kuhakikisha kombe linakuja Tanzania.


Mungu Ibariki Yanga, Mungu Ibariki Tanzania.


Chanzo: Dar24

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post