Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Walale sasa. Baada ya mapambano ya muda mrefu ya kivumbi na jasho, rasmi amepatikana tajiri aliyeshinda vita ya kuinunua Manchester United ikiwa ni baada ya miezi sita tangu kutangazwa kwamba timu hiyo inauzwa.
Kwa mujibu wa tovuti ya The Sun, Sir Jim Ratcliffe ndio aliyeshinda vita dhidi ya matajiri wengine na hiyo itakwenda kumaliza utawala wa familia ya Glazers ambayo imekuwa ikimiliki timu hiyo kwa zaidi ya miaka 18.
Taarifa ya kuuzwa kwa Man United ilitangazwa wakati wa michuano ya Kombe la Dunia kule nchini Qatar na mabosi wa timu hii walikuwa wanahitaji mtu anayeweza kuwekeza ama kuinunua mazima.
Kwa miezi kadhaa baada ya tangazo hilo vita ikabakia kuwa kati ya matajiri wawili ambao ni bilioni Muingereza, Ratcliffe na bilionea kutoka Qatari Sheikh Jassim Bin Hamad Al Thani.
Ripoti zinaeleza kwamba dau la Ratcliffe la Pauni 5 bilion ndio limeonekana kuwavutia zaidi wamiliki wa sasa wa Man United kwani mbali ya kupewa kiasi hicho pia watabakia kwenye timu wakimiliki sehemu ndogo ya hisa.
Inadaiwa mpango wa kwanza kwa familia ya Glazzer ilikuwa ni kuiuza timu hii mazima lakini wakati mchakato unaendelea baadhi ya wanafamilia akiwemo Joel na Avram Glazer wao walibadilisha mawazo na wakasema kwamba wanahitaji kuendelea kubakia kwenye timu hiyo hata kama wengine watauza.
Hadi sasa The Raine Group, ambayo ni benki iliyopewa tenda ya kuhakikisha wanaiuza timu hiyo na baadhi ya watu wa ndani kutoka benki hiyo wanaeleza kwamba aliye kwenye hatua hizo za mwisho ni Ratcliffe.
Awali ofa ya Sheikh Jassim ya Pauni 5 bilioni ndio ilikuwa kubwa zaidi kuwasilishwa mezani lakini changamoto ilikuwa ni kwamba walihitaji umiliki wa asilimia zote.
Inadaiwa kuwa kitendo cha wamiliki wa Man United kukubali ofa ya Ratcliffe huenda ikazidisha idadi ya matajiri wengine ambao wanaweza kuweka pesa na kununua hisa kwenye timu hiyo. Miongoni mwa taasisi ambazo zinataka kuweka pesa kwa ajili ya kuinunua timu hiyo ni Carlyle.
Licha ya mpunga ambao umewekwa na Retcliffe ni asilimia 50 za umiliki ambazo atapewa jambo ambalo bado litaipa nafasi familia ya Glazzer kuendelea kuingoza timu hiyo tena kwa nguvu sawa.
Hata hivyo mashabiki wengi hawaonekani kuridhishwa na dili hili kwani wengi wao walitaka kuona familia hii inaondoka kabisa kwenye uso wa Man United.
Lakini kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali ni kwamba hata kama watabakia kwa hisa zao baada ya kuiuza timu hii kwa Ratcliffe watakuwa na nguvu ndogo sana ya kufanya uamuzi wa mambo mbali mbali.
Ripoti ya hivi karibuni ya Sky Sports inadai kuwa kwenye mkataba baina ya Glazzers na Retcliffe kuna kipengele ambacho kinawalazimisha familia hiyo kuuza hisa zao zilizobakia mwaka 2026.
February mwaka huu Ratcliffe alisema: 'Tuna malengo makubwa na tunahitaji kuwekeza kwenye timu hii ili tuifanye tena kuwa moja ya timu kubwa zaidi Duniani, tunahitaji kusaidia timu iende kwenye kurasa nyingine kwa kuzingatia aina ya utamaduni wa soka la Kiingereza, tuifanye iwe ya kisasa zaidi na yenye kupitia mchakato, pia kuwapa mashabiki nafasi zaidi, tunataka kurudisha historia nyuma na malengo yetu hasa ni kushinda mataji makubwa kama Ligi ya Mabingwa."
Post a Comment